Mtandao wa Molly’s na Wafadhili wa Kimataifa. Mtandao wa Molly's ukifanya mafunzo na washirika wa shirika la Children in Crossfire Kwa upana sana wafadhili wanatafuta Asasi zinazofanya kazi hapa Nchini, Lakini wafadhili wengi bado wanaamini Mashirika ya Kimataifa yana uzoefu na kazi hizo kuliko Asasi za Kiraia na mashirika haya makubwa yana nafasi ya kuweza kufanya kazi za gharama kubwa kuliko Asasi za Kiraia za Tanzania. Kwa hali hii Wafadhili wa kimataifa wamekuwa wakitafuta Asasi za Kiraia zenye uwezo w juu kutekeleza malengo yao.

Ni changamoto kubwa kwao kuzitambua Asasi hizi na mara chache kuzisaidia kukuza na kujengea uwezo wao ili watekeleze mradi wao kwa ufanisi mkubwa na kufikia mahitaji ya mradi.

Kwa Asili ya uhusiano baina ya wafadhili na Asasi za Kiraia, huleta mambo mengi mojawapo ni kuona kama Asasi hizi hazina uwezo mkubwa kufikia malengo hasa kwa wafanyakazi wao wa kujitolea.

Japokuwa Wafadhili wengi wa Kimataifa hutambua mchango wa kujengea uwezo ili kazi sio za mradi lengwa pekee bali za Asasi nzima ni mara chache kukuta Asasi hawana nafasi ama muda wa kuweza kushughulikia masuala haya. Tunaweza kusaidiaje? Mtandao wa Molly’s husaidia Wafadhili wa Kimataifa kwa njia zifuatazo:

1. Huakiki Asasi zisizo za Kiserikali kwa ajili ya wafadhili wa Kimataifa. Uhakiki huu husaidia kuwapa Mwanga wafadhili wa Kimataifa wapi pa kufanyia kazi ili shughuli zote za Asasi ziweze kufanywa kwa weledi na hufanya hivi kwa njia ya mafunzo. Kutokana na uwezo wetu Asasi nyingi huwa huru kujadiliana nasi kuliko hata na wafadhili wao, kwa kuwa wao hutuona sisi kama tofauti na wafadhili wao.

2. Hutoa huduma za kujengea uwezo kwa Asasi hizi ili ziwe bora zaidi. Tuna utaalamu uliobobea katika kujengea uwezo Asasi hizi kama Asasi na kama kwa kiongozi mmoja mmoja.Mtandao wetu wetu una uzoefu mkubwa wa kazi hizi za kujengea uwezo.

3. Kuziunganisha Asasi za daraja la juu na la kati na wafadhili wa kimataifa. Tunawashauri wafadhili hawa juu ya kufadhili Asasi hizi kwa sababu ni bora na tuna furaha kutoa taarifa za kina juu ya Asasi hizi juu ya uwezo wao.