Paul Joynson-Hicks MBE Ameishi na kufanya kazi Afrika ya Mashariki tangu miaka 20 iliyopita, na kazi yake kubwa alikuwa mpiga picha. Wakati wa kazi yake hiyo aligundua mahangaiko na kutengwa na sababu hizo zilimfanya aanzishe Miradi tofauti tofauti kusaidia makundi haya.

Alianza na rafiki yake mmoja na mradi wa kwanza ulikuwa wa kusaidia Watoto wa mitaani huko Kamapla  Nchini Uganda, Mradii huu ulijulikana kama Simba Mariri Klabu na sasa inajulikana kimataifa kama Retrak.

Baada ya Muda alikuja Tanzaniana kuanzisha Mashindano ya mbio za mbuzi yajulikanayo kama The Dar es Salaam Charity Goat Races, na kwa kipindi hicho alikuwa amekusanya zaidi ya shilingi milioni 500 za kitanzania tangu kuanzishwa kwake.  Amefanya kazi na COOK huko Uingereza, alikuwa akikusanya simu zilizotolewa kama msaada huko Uingereza na kuzitengeneza na kuziuza Kariakoo na pesa zilizopatikana zilisaidia kulipa ada za Watoto wa kike waliokuwa mitaani.

Kwa kuongeza pia ameanzisha 'Wonder Workshop' kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo ambao hawakuwa na kazi yoyote zidi ya kuomba. Mradi huu ni kwa wale walemavu wanawake kwa wanaume kufanya kazi za ubunifu wa kutengeneza vitu kutokana na vitu chakavu vilivyotupwa kama vile chupa, karatasi, mbao na vyuma chakavu.

Paul ni Mkurugenzi mwanzilishi wa Mtandao wa Molly's, kutokana na ujuzi na uelewa wake wa masuala ya Miradi alikuja na wazo la kufanya upembuzi na kusaidia mashirika machanga yasiyo ya kiserikali kuweza kuwa na uweozo wa juu kutekeleza majukumu yao napia kuyaunganisha na fursa mbalimbali za nje na ndani ya nchi na hii ilikuwa mwaka 2008. Mtandao wa Molly's ulianza rasmi mnamo mwaka 2011 mwaka mmoja baada ya kifo cha mtoto wake wa kike kufariki katika ajali akiwa na umri wa miaka 2. Kumbukumbu yake bado inaishi ndani ya Paul katika kusaidi watu wasiojiweza. November mwaka 2011 Mtoto wa Malkia Prince Charles alimwalika Mr Paul na kumpa tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake katika kusaidia jamii ya Tanzania na tuzo hii ambayo hujulikana kwa kiingereza kama Member of British Emperor (MBE).


Godfrey Mramba meneja mwenza na Mtendaji Mkuu wa Basil & Alred, ambako yeye ni mhusika mkuu wa masuala ya ushuru na kodi. Kabla ya kuanzishwa kwa Basil & Alred, Godfrey alikuwa Meneja Mkuu na makamu wa Raisi wa Coeur Tanzania Limited, iliyokuwa inamilikiwa na Coeur d’Alene Mines Corporation (Coeur), mzalishaji mkubwa zaidi wa madini ya shabahuko Marekani.  Amekuwa na Coeur kwa miaka 15(miaka saba kati ya hiyo alifanya kazi kama Meneja mtendaji na kama mwana bodi wa Coeur Tanzania), kabla ya hapo alifanya kazi kama mkaguzi wa hesabu katika kampuni ya Ernst & Young huko Seattle.

Godfrey ni Mkaguzi wa masuala ya hesabu na amehakikiwa (CPA) leseni yake ilitolewa huko Washington, Marekani, pia ni mwanachama wa taasisi ya uhakiki wa wakaguzi wa hesabu (AICPA) and the Washington Society of Certified Public Accountants (WSCPA). Pia amesajiliwa na kuhakikiwa na bodi ya wakaguzi wa hesabu hapa Tanzania (NBAA) vile vile amesajiliwa na Taasisi ya ukusanyaji wa kodi  kama mshauri wa masuala ya kodi. Ana shahada ya uzamivu ya masuala ya uhasibu aliyoipata huko chuo kikuu cha Idaho huko Marekani. 

Godfrey ni mwanabodi wa makuampuni na mashirika mbalimbali hapa Tanzania yakiwapo mashirika yasiyo ya kiserikali, mahoteli, Bima, uwekezaji na uzalishaji. Kama Mkurugenzi wa Bodi ya Mtandao wa Molly's, analeta weledi wake hasa kwenye masuala ya fedha na usimamizi bora kabisa.


Aida Kiangi Mkurugenzi wa shrika la kimataifa lijulikanalo kama ActionAid HAPA Tanzania. Ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya maendeleo ya jamii na ujuzi wake umejikita zaidi kwenye masuala ya mpango mkakati, upangaji na uendeshaji wa shirika na Utawala wa fedha serikalini na kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali, hasa hasa serikali za mitaa na kwenye asasi zisizo za kiserikali.

Kazi zake zilizopita ni pamoja na Meneja mikataba wa miradi ya PEPFAR kwenye shirika lijulikanalo kama Deloitte Consulting (kwa niaba ya USAID/Tanzania), Meneja Ruzuku toka chuo  kikuu ICAP-Columbia athapo hapo  Deloitte Consulting, na Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii pale Barrick Gold Tanzania. 

Aida ni mwanzilishi wa Young Executive Stars Tanzania (YES! Tanzania),mtandao wa vijana wakurugenzi kutoka sekta mbalimbali kama vile biashara, Serikalini, asasi zisizo za kiserikali, Elimu, jamii na sanaa ambao wanawawezesha wakuu hao kuendelea kuunganishwa pamoja ili kujifunza na kuwa viongozi bora zaidi.  

Analeta ujuziwake mkubwa wa kushirikiana na Asasi zisizo za kiserikali kwenye boadi hii ya wakurugenzi kwenye mtandao wa Molly's.


Aisha Sykes ni Mwanzilishi na meneja mwenza wa Refine Advisory, shirika lililojikita katika kutoa huduma za ushauri kwenye sekta ya uwekezaji katika jamii, maendeleo endelevu, mpango mkakati na kwa mashirika yasiyo ta kiserikali. 

Amefanya kazi na mashirika mbalimbali Afrika Mashariki ikiwamo na Ubalozi wa Kanada, Umoja wa Mataifa masuala ya wakimbizi, Twaweza, Jicho bunifu. Pia yupo katika mitandao mbalimbali kama vile Incite (Afrika ya Kusini), na amefanya kazi na mashirika kadhaa kwenye masuala ya ushauri  has katika sekta isiyo ya Kiserikali.  Aisha maewekeza nguvu zake katika kuhakikisha masikini waishio Afrika Mashariki wanapata hali nzuri na haya yote ameyafanya/anafanya kupitia asasi zisizo za Kiserikali.

Aisha ana shahada ya uzamivu katika masuala ya Sera na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha London Uingereza na ana shahada ya kwanza ya masuala ya Jinsia na sayansi ya Jamii aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town huko Afrika ya Kusini.


Catharine Joynson-Hicks, Mwana mazingira wa Kiingereza, amekuwa akiishi Kenya toka utoto wake na ameishi na kufanya kazi hapa Tanzania kwa muda wa miaka 13 sasa. Ana shahada ya uzamili ya masuala ya misitu na mazingira na uzoefu usiopungua miaka 20 wa makazi na viumbe hai, na amefanya kazi nchi zaidi ya tatu Tanzania, Kenya, Uganda na Msumbiji.

Mwaka 2001 alianzisha na kuiongoza asasi iliyojulikana kama, Sea Sense, na amekuwa akifanya kazi na jamii,  Serikali, na sekta binafsi pamoja na wanasayansi kuboresha sekta ya maji na utawala wake. Kwasasa ni mmoja wa wataalamu wa bodi ya ushauri ya Sea Sense. Catharine anaishi Arusha (Kasazini mwa Tanzania) na mumewe na watoto wawili wa kiume.

 

 


 Kennedy Oulu ni Mtafiti, mwana mkakati mtathmini na kiongozi, ana uzoefu wa miaka 12 katika sekta hizo tajwa hapo juu. 

Ana uzoefu Mkubwa sana na Asasi zisizo za Kiserikali, sekta binafsi na mawakala wa Serikali na amebobea kwenye masuala ya Vijana, wanawake na kwenye makundi yaliyo sahaulika kwa ujumla wake. Amefanya kazi katika Nchi mbalimbali zikiwamo Kenya, Malawi, Tanzania na Afrika ya Kusini kama mshauri mtaalamu  na kiongozi.

Alikuwa Mtendaji Mkuu mkazi wa shirika la The Foundation For Tomorrow (TFFT) mpka Januari 2016, na kabla ya hapo alikuwa Meneja wa ufuatiliaji na tathmini wa Restless Development Tanzania [2009-2012], na baada ya hapo alikuwa mshauri wa ufundi wa VSO huko Malawi. Pia ni mwakilishi wa Bodi wa TFFT.

Ken sasa hivi anafanya kazi ya kujengea uwezo Asasi zisizo za kiserikali, sekta binafsi na Umoja wa Mataifa na Serikali. na sasa anamalizia masomo yake ya shahada ya pili katika masuala ya utafiti, Elimu na Utafiti wa Jamii kutoka chuo kikuu cha London Uingereza.


Stephen Lumati
Assessment Panel Member

Stephen Lumati is an experienced teacher and education manager with 27 years’ experience both in the Government and in the NGO sector. He has a proven track record of providing exemplary leadership in teacher education; capacity development; quality assurance & standards; fundraising and grants management. He has worked as an Education Project Coordinator with Universal Intervention and Development Organization (UNIDO) in South Sudan. Prior to this, he worked as a Deputy District Education Officer with the Ministry of Education Kenya and as an Assistant Lecturer in various teacher colleges in Kenya. He is currently serving as the Scholarship and Mentoring Program Director at The Foundation For Tomorrow. Stephen is keen to use his experience, knowledge and expertise in creating positive social impact.


Razi Latif ana uzoefu wa miaka zaidi ya 20 wa masuala ya Maendeleo hapa Afrika, Asia, Ulaya Mashaiki, Mashariki ya Mbali na Urusi. Amefanya kazi kwenye Serikali moja katika Nchi zinazoendelea, Benki ya Maendeleo, Asasi zisizo za kiserikali, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Kwasasa ni mshauri wa masuala ya mazingira huko Uingereza (DFID).  

Razi aliwahi kufanya kazi Tanzania kwa muda wa miaka sita (6) Kenya mitano (5) ambako alikuwa akifanyakazi kwenye masuala ya uoto wa asili, Maendeleo vijijini na kwenye Miradi ya mazingira na wafadhili na washirika mbalimbali. Pia amefanya kazi za kufanikisha ruzuku na misaadachini ya harakati za the 'One-UN'. Wasifu wa Razi ni kwenye masuala ya usalama majini, udongo, siasa na uchumi.

 Jeremy Cross ni mtafiti kwa miaka 25 akiwa amebobea kwenye sekta binafsi, Asasi zisizo za Kiserikali na amefanya kazi sehemu mbalimbali Afrika na Uingereza. Ameishi Tanzania kwa miaka saba (7) ana uelewa mkubwa sana wa jinsi uendeshaji wa shughuli ulivyo hapa Tanzania hasa kwa asasi ndogo ndogo na jinsi zinavyofanya kazi kama zile zinazofanya kazi na Mtandao wa Molly's. Tangu mwaka 2010 amekuwa anifanya kazi na Comic Relief kama mtathmini binafsi akitoa ushauri kwa wakazi waishio mijini kwenye maeneo fungamani na sasa nafanya kazi kama Meneja wa mtandao wa kimataifa kwa Prince’s Foundation kwa kujenga jamii.

 Lady Gill Brentford

Gill alizaliwa Kenya lakini alikulia Uingereza; ameolewa na ana watoto wanne. Ni mtaalamu wa masuala ya Uhasibu na Biashara na amekuwa kwenye bodi za Udhamini tangu akiwa na miaka 25 baadhi ya bodi hizo zipo na ofisi Afrika. Amewahi kuwa Kamishna wa Church Commissioners wa Uingereza na Raisi wa  of CMS kw nyakati tofauti.

 

 


Julia Maria Angeli ni Mkurugenzi Mtendaji mpya. amekuwa akifanya kazi kwenye sekta ya Maendeleo kwa miaka saba sasa huko laya na Asia na Afrika vile vile. Mnamo mwaka 2012 alimaliza shahada ya azamivu na kubobea katika masuala ya jinsia na Maendeleo na ujuzi huu aliupata huko Uingereza. na utaalamu wk umegubikwa na utalamu wa masuala ya mpango wa uzazi na afyaya uzazi na amefanya kazi katika mashirika mbaimbali yakiwemo Marie Stopes International na UNFPA. pia an utaalamu katika mauaa ya utafiti na programu na ni mhamsishaj wa ufanisi na ubunifu katika mipango na uwezshaji na hivi karibuni alikuwa akijengea uwezo mashirika madogo ya kitanzania yanayofanya kai hapa Dar es Salaam Tanzania. Amekuwa aiishi Tanzana kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja sasa na amejidhatitikusaidia kujenga uwezo wa asasi zisizo za kiserikali hapa Nchini.


Nestory Mhando
Programme Manager

Nestory Mhando is Molly's Network new Programme Manager. He has worked for nearly nine years with civil society organisations in Tanzania and has supported them to develop programmes, manage projects, set strategic directions and improve monitoring & evaluation systems. When working for the Foundation for Civil Society he conducted organisational capacity assessments and provided training and mentorship to his grantees. He also has extensive experience in engaging with various stakeholders from the local community, Local Government Authorities, development stakeholders and the donor community.


Allen Charles
Finance & Admin Officer

Allen Charles is Molly's Network new Finance & Admin Officer. He completed his MBA in Finance at Iringa University and also completed a B.A. in Account and Finance at the Institute of Finance Management in Dar es Salaam. His professional experience includes working for international NGOs, having worked as a Project Accountant for World Wide Fund in Iringa from 2012 to 2016. He also worked as a Project Accountant with the Training Centre for Development Cooperation in Eastern and Southern Africa (MS-TCDC) from 2007 to 2012. He has extensive financial experience and has also been trained in risk management, grant management, project planning and monitoring and evaluation.