Kila mara Mtandao wetu huulizwa ni namna gani tumeweza kutengeneza mpango huu na vitendea kazi tunavotumia wakati wa mchakato wa utambuzi na utathmini, nani tumemshirikisha kutengeneza mchakato huu.

Vyote uthubutu na kuongoza kwa mfano na kwa uwazi na kujitambua kwa kushiriki mchakato huunumesaidia upatikanaji wa vitendea kazi hivi tuvitumiavyo wakati wa mchakato mzima. na bado tunaendelea kujifunza na kuendeleza mchakato huuna kwenye imani hii tunakaribisha maoni naushauri toka kwa yeyote mwenye nia kama yetu.  

Mtandao wa Molly's Ulitengeneza hatua za awali za uchambuzi mnamo mwaka 2011, kwa kufuata msingi wa mchakato huu uliokuwa ukifanyika huko Mashariki ya mbali (Philippines) uchambuzi huu ulikuwa unafanywa na Mfanyakazi mmoja wa mtandao wa Molly's na ufaulu wa asasi ulitegemea zaidi na idadi ya ''ndiyo'' na ''Hapana'' na uamuzi wa kusema asasi hii imefanya vizuri na kupata utunuku.Molly's.  Na maswali mengi yalikuwa ya kiwango cha chini cha uhalali wa kufanya kazi hapa Nchini, na kati ya mwaka 2011-2013 Mtandao ulipitia mashirika zaidi ya 70.

Julai mwaka 2013 Mtandao wa Molly's ulipitia upya uchambuzi uliokuwa umefanyika hapo awali ili kujifunza ni maeneo gani hatua za uchambuzi zilifanya kazi vizuri, na maeneo gani yafanyiwe kazi zaidi.

Tulihitimisha kwa kusema mchakato huu ni muhimu (Kusaidia asasi kutambua mambo mbalimbali),lakini kitendea kazi chetu hakikuwa kinaleta majibu mengi ambayo yangesaidia kusaidia mashirika haya. kwa miaka miwili ya mwanzo ya Mtandao kwa kuwasiliana na wafadhili wa ndani na nje ya Tanzania tulugundua kuwa: Mchakato ulipaswa kuwa wa ndani zaidi ili kupata tulichodhani kingesaidia asasi zetu. 2) Muhuri wa Mtandao haukupaswa kutolewa kwa jinsi maswali ya NDIYO na HAPANA tena kwa maswali ya kiwango cha chini ili kupata ufadhili wa nje na ndani. 3) kutowezesha asasi ambazo hazijakidhi kiwango lakini zina maono ya mbali na zina tabia ambazo zinaweza kufanya zikafuzu mchakato huu ndani ya muda mfupi.

Mnamo mwezi wa Oktoba 2013 tuliingia katika utekelezaji/ushirika wa Pamoja na the Good Governance Group Foundation (G3F).  Ambao ni wataalamu wa masuala ya uunganishaji wa masoko walitoa wafanyakazi wao waanzilishi wa Good Governance Group Limited (G3), ambao walijitolea kufanya kazi nasi na hujitoa kufanya kazi dunia nzima.

G3 ilileta maarifa yake  kwetu hasa kwenye masuala ya sera za rushwa, utambuzi wa asasi na viwango vya kueleweka kama asasi na haya yaliletwa kwa sababu ya ujuzi wa miaka mingi ya kazi hapa Tanzania Kwa Pamoja walifanya kazi nasi kupitia upya hatua zetu na utaalamu tuutumiao kufanya uchambuzi.

 

  1. Njia za uchambuzi wenye tija kwa kupitia hatua mtambuka na za wazi na pia za kimkakati katika kukusanya vielelezo. 
  2. kujenga Uweledi na utaalamu kutoka kwa wachambuzi wa kujitegemea  na namna gani mbinu hizi zilitumika na zimetumika kuelezea juu ya umuhimu wa kazi hii na
  3. kusaidia kamati ya uchambuzi kufanya maamuzi yasiyofungamana na upande wowote.

Mtandao wa Molly's umetengeneza Mpango Mkakati wake wa miaka mitatu 2015-2018. Mpango Mkakati huu unaonyesha dira na malengo, unakaribishwa sana kuusoma, Karibu ujipatie nakala hapo chini!