Kuna maelfu ya asasi zisizo za kiserikali hapa Tanzania, kuanzia za mtu mmoja mmoja mpaka zile za kimataifa.  Kuongezeka huku kwa wingi wa asasi zisizo za Kiserikali kumefanya kuwepo na ukuaji wa kiuchumi na sera za kijamii hivyo kupelekea kuwepo na hitaji la uwajibikaji toka kwa wahisani wa nje na ndani ya Tanzania. Asasi hizi zimeonekana kuwa rahisi kufikisha mahitaji kwenye jamii kuliko makundi mengine.

Hitaji la kuanzishwa kwa mtandao huu wa kwanza hapa Tanzania uligunduliwa na mwanzilishi wa mtandao huu Bwana, (Paul Joynson-Hicks). Alipotaka kuchangia kiasi kidogo cha pesa kwenye shirika au asasi isiyokuwa ya Kiserikali kupitia mbio za mbuzi zijulikanaz kama the Dar es Salaam Goat Races (moja kati ya matukio makubwa ya uchangishaji wa fedha hapa Tanzania),hakuweza kutimiza malengo kwasababu hakuweza kutambua asasi zilizokuwa na vigezo.  Alikusanya washauri mbalimbali toka kwenye asasi na wafadhili wakubwa na wazo la kuanzishwa mtandao wa Molly's lilizaliwa hapo.

Tokea hapo Mtandao wa Molly's umeweza kukutana na washirika mbalimbali kama vile Makampuni ya ndani na nje ya Tanzania, washirika wa maendeleo wa ndani na nje ya Tanzania na asasi zisizo za kiserikali,  na watu mablimbali na mawazo yao ndiyo yaliyofanya leo hii mtandao wa Molly's kuwa kama tulivyo.

Tumefanya utafiti wa moduli mbalimbali zinazotumika kwa sasa na kujifunza toka kwa wengine namna ya kufanya utoaji wezeshi We have (mfano. AusAID and The Philippine Council for NGO Certification); Asasi zisizo za Kiserikali kwenye uwzeshi wa kujitegemea (mfano Mchango wa seal huko Ujerumani na msaada wa nje.com wa Marekani); na faida kubwa zaidi za mtandao huu ni kuongeza imani na uaminifu kwenye jamii, washirika wa maendeleo, pia huwezesha uwezo wa kiutawala na fursa za watoa ruzuku.

Kutokana na  matokeo hayo, tumeweza kuanzisha asasi huru ya kwanza hapa Tanzania inayofanya  masuala ya kujengea uwezo mashirika yasiyo ya kiserikali hapa Tanzania kupitia upembuzi yakinifu toka mwaka 2011. Baada ya miaka miwili ya utendaji kazi, tuliweza kuiboresha kwa mapana  moduli yetu na kuanza kujengea uwezo asasi zilizofanyiwa upembuzi yakinifu, asasi hizi ni zile zilizoonyesha uwezo wake kiutendaji lakini zilikuwa bado hazijafikia uwezo wa juu kabisa kiutedaji.

Mtandao wa Molly's umepewa jina hili toka kwa mtoto wa kike wa Paul na Catherine Joynson Hicks ambaye alifariki kwenye ajali akiwa na umri wa miaka miwili, hiyo iliwafanya Paul na Catherine Joynson Hicks kufanya jambo hili la kuleta mabadiliko katika asasi zetu ndipo walipoanzisha Mtandao wa Molly's mwaka 2011.

Mtandao wa Molly's ndilo jina na lililosajiliwa na linalotumika kwa kazi zote zifanywazo na mtandao huu

Mtandao wa Molly's na kazi zake zinasimamiwa na jina hilo hilo lililosajiliwa lakini uchambuaji wa mashirika hufanywa na kamati teule ambayo inajitegemea.