Mtandao wa Molly's unaamini kuwa jamii wana uelewa mkubwa wa mahitaji yao ndani ya jamii husika. Mara nyingi wapo katika nafasi nzuri ya kukabilianan na changamoto zinazoikabili jamii husika na namna ya kuzitatua changamoto hizo. 

Jamii hii pia ina juhudi katika kuleta Maendeleo ya jamii husika, kwa njia za kibunifu na kisasa kuhusu masuala ya Maendeleo endelevu.

Lakini asasi hizi hazijaunganishwa na fursa, hazina rasilimali watu na rasilimali fedha na pia ueledi au maarifa na njia muafaka bado si nzuri katika uendeshaji na uendelezaji wa asasi hizi.

Mtandao wa Molly's upo mahususi kusaidia watu hawa na asasi zao kufanikisha shughuli za asasi hizi zinaendeshwa kiueledi zaidi na mtandao huu hufanya hivi kupitia utathminishaji wa asasi hizi na pia katika kuzijengea uwezo wa kutekeleza kazi zao kama walivojipangia.

Dira ya Mtandao wa Molly’s:

Kuwapo kwa utambuzi wa mchango wa asasi zisizo za kiserikali katika Maendeleo kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya Taifa katika kuleta Maendeleo.

Malengo mahususi: 

Ni kusaidia Asasi zisizo za kiserikali hapa Tanzania kuwa zenye ufanisi na kutekeleza majukumu yake na hii ni kupitia mpango wetu wa kujitegemea kwa kufanya upembuzi na kujengea uwezo Asasi hizo.

Malengo yetu:

1. Asasi zisizo za Kiserikali hapa Tanzania zinavutia ubia, fursa kutoka kwenye mashirika ya kimataifa na ya kitaifa.

2. Asasi za kitanzania "zenye uwezol*" zina maarifa ya kutosha, njia muafaka kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.

3. Kuna mtandao hai wa wanachama wanaonufaika kutokana na kujifunza mambo mablimbali toka kwa wengine.

*"Mashirka yenye uwezo wa kati" yanakidhi vigezo vya mtandao wa Molly's lakini si vigezo vyote.